Unakumbuka enzi zile (wale tulioiishi enzi hizo,ingawa sasa nasikia katabia haka kameanza tena)za kwenda kwenye majumba ya sinema kuangalia sinema mbalimbali? Nakumbuka majumba ya sinema yalikuwepo mikoa mingi Tanzania inagawa dari salama yalikuwa mengi akina Drive in, (hapa kama ulikuwa hunakitu unaangalia sinema bubu...nitarudi kwenye hili),New chox,empire,Avalon. Kule mwanza nasikia kulikuwa na majumba mawili ya sinema nakumbuka moja tu Liberty, mji Kasoro Bahari nayo kulikuwa mawili nakumbuka Sapna, huko mbeya au Iringa nako kulikuwa na....mmh nimesahau. Basi enzi hizo nakumbuka kulikuwa na mabingwa wa kusimulia zile sinema hata kama mliiona wote basi mtaanza kusimuliana tena...tena na tena hata kama wengi wetu wakati huo hata kimombo hatujui basi utasema kila kitu jamaa walivyokuwa wanasema kwenye hiyo sinema...au wakati wa sinema yenyewe watu watapiga makelele..angalia nyuma wewe!!!jamaa anakuja kukuua! au kama pale Drive in kwa nje, jamaa anakusimulia kama anasikia vile. Ilikuwa raha mstarehe bwana enzi hizo nakwambia kama ni shule basi wanafunzi wote wanaweza kuja kama kuna sinema maarufu mjini na wakakusimulia mwanzo hadi mwisho lakini hawajaiona wao ila wamesimuliwa lakini wanakusimulia bila kukosea (ndio na kuongezea chumvi...he! he! he!)
Lengo langu basi mimi leo ni Kukusimulia moja ya sinema ambayo inanifikirisha sana mpaka leo hii sinema sasa nimeisha iangalia mara tatu. Sinema hii inakufanya ufikiri zaidi kwa mambo mengi yanayotokea katika nchi zetu (wao wanaziita zinazoendelea).
Sinema hii inaitwa The constant Gardener.
Sinema hii inaanza kwa kuonyesha watu wawili walioingia katika mapenzi ya ghafla baada ya kuoana wanafunga safari kwenda kuishi afrika(kenya) Kwa sababu Bwana na mfanyakazi wa serikali ya Uingereza,baadae Bibi anauwawa pamoja na Dereva wake mwafrika(inapakazwa kuwa mumewe ndio kamfanyizia kwa sababu ana husiano wa kimapenzi na huyo mwafrika) ..basi Bwana ndio anafanya kazi ya kupeleleza kwanini kipenzi chake kimeuwawa anakuja kugundua kuwa mkewe alikuwa akichunguza uharamia ambao makampuni ya madawa yalivyokuwa yakifanya kwa kutumia wananchi bila ya wao kujua kama mahabara zao ,yaani kujaribia madawa yao.
Hii sinema inaelezea makampuni ya madawa ambyo yanajaribu madawa yao kwenye nchi zetu masikini kwa sababu watu hawa hawana faida yoyote kwao na kwasababu viongozi wao pia hawawajali raia wao.
Ni kweli magonjwa yamekuwa mengi na watu wanaitaji dawa lakini utaratibu wa kupata dawa inayotibu ni mrefu na wa gharama kubwa hivyo makampuni yanatafuta njia nyingi za kupunguza gharama na urefu huu kwa kututumia sisi tusio na uwezo na waangalizi wetu wanatuuza. Mara ngapi umesikia dawa za Malaria zimeingia Tanzania baada ya muda unaambiwa hazifai, zinaletwa dawa za kila aina kwa kila magonjwa baada ya watu kupona wanadhurika halafu zinaondolewa jiulize inakuwaje hapa? Kuna mchezo mchafu sana tuanachezewa hapa inabidi kuwa makini sana ....kama hujaiona hii sinema naomba uitafute uiiangalie kama umeiiona iiangalie tena !
3 comments:
Sijaiona bado hii sinema uliyoizungumzia.Nitaitafuta.
Lakini Mzee umenikumbusha mbali. Wakati niko shule ya msingi nilisoma na Jamaa aitwaye Mambo. Sijui yuko wapi!Huyo jamaa ndio alikuwa msimulizi wetu wa sinema.Ila alikuwa na uwezo wa kuisimulia sinema kiasi kwamba hata kama umeiona hauwezi kuifaidi kuliko akikusimulia yeye.Siku nyingine tulikuwa tunachelewa kuondoka shuleni , darasa zima, kisa anatusimulia sinema za kihindi. Yeye hajui kihindi lakini atakusimulia yote Mituni Chakaraboti asemayo na afikiriayo. Utasia halafu Mituni akasema sasa basi!Leo utakiona! Umenikumbusha mbali Mzee!Asante!
Simon itafute hii sinema ujioone mwenye. Nilipita pale kwako siku moja nikaona umeandika kuhusu Ukoko basi nilitaka kutoa mchapo mmoja wa ukoko nikashindwa kuacha ujumbe kwako.
Sijabahatika kuiona hiyo sinema. Ila nalaumu sana jinsi bara letu la Afrika linavyogeuzwa kama uwanja wa majaribio na pia jalala la vitu visivyofaa.
Tumemeza sana Klorokwin, then A.S.P, sijui nini tena sasa hivi. Yaani mambo ni hobelahobela.
Nitaitafuta hiyo sinema.
Post a Comment