Tuesday, February 13, 2007

UBEPARI & other kids stuff

Huyu jamaa kanifikirisha sana, anasema kwa kipindi tunachoiishi sasa duniani kuna maendeleo ya tekenolojia kuliko vipindi vyote lakini ikitakiwa kifanyike kitu kimoja cha maana kama kulisha watu walio katika shida inakuwa... mmhh
Anasema jamaa wa magharibi hawana maji kukatika, watoto wanakwenda shule ,kuna kujisika salama lakini je wanajisikia vizuri?
Anasema ubepari ni kama gari bovu ambalo viongozi wanalitengeneza lakini halitengemai wewe unalipia lakini gari lako halitengemai...
Anasema yeye hataki mchango wako bali anataka wewe ujiulize maswali ya hali ya mambo duniani....
Anatoa mfano wa jinsi watoto wakiwa wanacheza huwa wanagombana lakini hupatana baada ya muda mchache lakini hawa watoto ukumbuke hawajajifunza diplomasia yausuluhishi wala nini...inakuwaje huu utaratibu unavyokuja kuharibika na maana yake nini nini?...
Na mambo kadha wa kadha.
Basi msikilize huyu jamaa (anaelezea kwa muda mrefu kidogo hivyo inabidi uwe na muda wa kumsikiliza) ,fuata maelezo yake kwa kumsililiza moja kwa moja kupitia viungo alivyoweka nenda pale anapokuwambia watch online . Huyu jamaa anapatikana hapa. Mimi nakubaliana nae kwa mambo mengi tu aliyoyasema.

4 comments:

mwandani said...

kuuzungumzia ubepari vibaya siku hizi imekuwa kama dhambi na ukiusifia ujamaa unaokana kama vile ni mtu aliyepitwa na wakati. Ukweli ni kwamba mara nyingi mabepari wana hulka za unyang'anyi.

Hivi majuzi nilisikia wale wawekezaji kwenye madini - wanaoongeza tarakimu za pato la taifa kwamba wanatupunja sana. Sasa taifa lenye kujali jamii lingeongeza pato la taifa kwenye hayo madini na kutumia vizuri kwenye shughuli za kijamii. Taifa linalosema tugawane sawa tusipunjane - utasikia likitengwa kinamna na kupakaziwa. Venezuela na Bolivia kama mfano.

MTANZANIA. said...

Huu ndio UBEPARI. Kama ulivyo mchezo wa watoto, mtoto mjanja ndiye atakayewapunja wenzake mara zote. Vivyo hivyo hata ktk uchumi wa kibepari mjanja na mwenyenacho ndiye atakayeendelea kujiongezea kupitia mgongo wa asiyenacho na ambaye anazidi kutokuwa nacho. Hapa kuna kazi!!!

Anonymous said...

Mwandani kasema kweli. Imeonekana kama vile dunia nzima tumekubaliana kuwa ubepari ndio mfumo bora na sahihi wa kiuchumi na kisiasa. Uongo huu. Matatizo ya kijamii yaliyoko katika nchi vinara vya mfumo huu huwa yanafichwa na picha za filamu, video za muziki, utamaduni maarufu, akina CNN na Ebony Magazine, majumba makubwa yanayokaribia kugusa anga, n.k. Lakini ukitazama undani wa maisha ya raia katika nchi hizi utakuta hawana furaha kabisa. Wanaweza kuwa na raha (kama ulivyosema Ndabuli: maji hayakatiki, umeme wanao, watoto wanakwenda shule) lakini furaha hawana.

Nchini kwetu inaelekea kama vile mjadala wa itikadi inayotufaa umeshafungwa. Wazungu, kupitia benki yao ile na lile shirika lao la fedha, wametuambia kuwa ubepari ndio unatufaa, viongozi wetu wakasema, "ndio mzee." Wananchi tukatazama tukaona majumba makubwa makubwa, mahoteli tuliyokuwa tukiyaona kwenye sinema, magari ya milango sita, redio na vituo vya luninga kibao...basi tukasema, "kweli nchi inaendelea."

Anonymous said...

Du, kweli hapa mmeniacha hoi! Hivi, hebu fikiri kuhusu nadharia hii hii ya Kijografia:
Upepo huvuma kutoka katika eneo lenye mgandamizo mkubwa wa hewa kwenda kwenye mgandamizo mdogo wa hewa. Baadaye sehemu yenye mgandamizo mdogo wa hewa hugeuka kuwa sehemu yenye mgandamizo mkubwa wa hewa, baada ya hapo upepo hugeuka na kuelekea kule kwa mwanzo ambako sasa kumekuwa na mgandamizo mdogo wa hewa.

Kwa kutumia nadharia hii: katika tambo kubwakubwa za nyakati (mfano miaka 200 - 500) mfumo fulani unaweza kutawala dunia. Kwa mfano, hivi sasa dunia haina budi kutawaliwa na ubepari mpaka usambae kote kabisa. Watu fulani wajilimbikizie mali wee mpaka wachoke. Wale wasio na mali waonje chungu na tamu ya mfumo wa ubepari. Baada ya hapo watu hawa wa chini lazima watachoka, watageuka na kuleta mapinduzi (Marxism?). Mapinduzi haya yataleta Ujamaa utakaosambaa duniani kote na watu kugawana yale yaliyopatikana. Baada ya hapo (Animal Farm) wataanza kujitokeza mabepari wajanja (sorry walio more equal kuliko wengine) hawa wataanza kujilimbikizia tena mali. Hatimaye Ujamaa unakufa tena. Basi inakuwa ni mzunguko wa namna hiyo. Usiku na Mchana.

Tafakarini.