Saturday, September 15, 2007

GLOBAL PUBLISHERS MMMMH !!!?? HADITHI HII KAWAFUNDISHA NANI?

Si Kawaida yangu kuanza kaundika jambo linalonikera ghafla lakini hili nimeshindwa kuvumilia. Nilipata kukutana malumbano kati ya Chahali na watu wa Globalpublishers wa Tanzania.
Katika malumbano yao niliona bwana Chahali akiwa na hoja nyingi zenye msingi katika hilo swala waliliokuwa wakibishania(kwa upande wangu). Ingawaje nilikuwa msomaji tu lakini maoni yao wote yalikaa kichwani mwangu.
Kilichotokea sasa ni ijumaa moja ya gazeti linalochapishwa na globalpublishers lilitoa picha ambayo ilileta utata (hasa kwangu mimi) na wengine kuhusu uwezo wa watoa habari hawa kwani hizo picha nilipata kuziona kitambo sehemu nyingine. Kilichonishtusha ni kuwa zilitumiwa kama ni habari mpya iliyotokea huko nyumbani. Baada ya kusoma hizo habari nilisema kweli sasa tumekwisha...yaani hawa wachapishaji wanafanya kitu kama hiki? Nikamkumbuka Chahali ni kasema hapa hana tena la kujitetea ni kuacha mwenye macho atazame. (Chahali nakuunga mkono aslimia 200! kwa magazeti ya Udaku). Kweli kwenye uongo ukweli ujitenga.
Nashukukuru kwa watu wengi kuwatolea macho hadi wao wamefuatilia hilo swala na kulifanyia kazi soma hapa na hapa.
Inatia aibu sana na ndio maana nilaandika kuwa ni vizuri mara nyingi kujiuliza Hadithi hiyo kakufundisha nani?

Thursday, September 13, 2007

WADUDU NA MADEREVA NA JAMII

Inasemekana sisimizi au siafu au nyuki hana uelevu sana kama inavyofikirika kuwa nao. Ila kundi la sisimizi/siafu/nyuki ndio linauelevu (umenipata hapo?)... Yaani hilo kundi linaweza kutatuta tatizo ambalo kama huyo sisimizi/siafu/nyuki angekuwa peke yake isingewezekana. Kama kutafuta njia fupi ya kwenda kutafuta chakula, kuwapanga wafanyakazi kwa kazi ,mbalimbali au kuwa walinzi wa sehemu waishiyo. Yaani wakiwa mmoja mmoja wanakuwa madunya ila wakiwa pamoja wanachangamkia tatizo haraka na kwa makini kwenye mazingira yao. Kufanya hadithi fupi ni kuwa watafiti wa wadudu hawa wamegundua kuwa hakuna ambayo ndio Kiongozi ila maamuzi yanategemea na jinsi wanavyo wasiliana. Soma hiyo habari hapa.
Utajiuliza sasa ikiwa hivyo ndio nini? Mimi napenda kuhusisha tabia hiyo na ule utaratibu wa madereva (Wa Tanzania) kuwashiana taa, yaani wanapeana ishara pale magari yanapopishana ndio wanawasiliana kuwa nanukuuu maandishi ya Ndesanjo kuwa,"katika zile alama za madereva kuna alama za kuashiria kuna "mkusanya kodi" mbele (yaani askari wa "usalama" wa barabarani (au usalama wa mfukoni). Halafu kuna ishara ya kuwa kuna "vichwa" (yaani abiria huko alikotoka". Yasome hapa. Sasa sijapata kuja lipi ndio huwa ni zaidi. Kwa mtazamo wangu madereva waliweza kujigundulia utaratibu mzuri sana wakupashana habari ya nini cha kufanya baada ya kuwashiana taa. Wao wako kama hawa wadudu na ukiwa peke yako huna ujanja ila mkiwa wengi mnaweza kupashana habari kuepushana na unaloliona wewe kuwa ni Shari.
Lengo la hadithi hii ni kukandamizia kuwa kuna njia nyingi za kusaidiana ili kuondoa tatizo kama wanfanyavyo wadudu au madereva (ila siwaungi mkono kwenye swala la kupindisha sheria za barabara)...Umenipata hapo?