Sunday, October 08, 2006

WARUSI MHH..NINA WASIWASI!

Jumamosi ya tarehe 7 oktoba 2006 nimesoma na kusikia kuwa mwandishi mmoja wa habari wa urusi Anna Politkovskaya ameuwawa kwa kupigwa risasi bonyeza hapa kusoma inasemekana mwandishi huyu wa habari alikuwa mstari wa mbele katika kuandika habari za ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Urusi. Na ni wiki hiyohiyo ambapo kulikuwa na mtafaruku kati ya serikali ya Urusi na Georgia uliosababisha Urusi kuwarudisha nyumbani wa georgia kibao kwao bonyeza hapa kusoma. Haya matukio hasa hili la kuwarudisha wageorgia limenifanya nikumbuke unyama ambao warusi wanawafanyia wageni hususan wanaotokea Afrika au weusi (Peter Tosh mwanamuziki wa miondoko ya reggae aliimba mwimbo mmoja unaosema as long as you are blackman you are an African,no matter where you are coming from,Bonyeza hapa usome beti za wimbo huo. Haijali unatokea wapi,iwapo wewe ni mweusi ni mwafrika) Huko Urusi hasa mji wa st.petersburgh watu weusi wamekuwa wakiuwawa kwa wingi na bila ya watu kupiga makelele kama yanayopigwa sasa bonya hapa kusoma. Sipingi watu kupiga Kelele ila naona kelele zenyewe zinapigwa kwa kuangalia rangi. Najua kuwa sehemu nyingi duniani hali ndivyo hivyo ilivyo lakini, Juzijuzi raisi Urusi alifanya safari ya Afrika (kuna mwanablogu mmoja au Habri mmoja sikumbuki nilisoma wapi waliipa jina habari hiyo the scramble for Africa) na hakuna sehemu niliyosikia kuwa hili jambo likizungumzwa. Ndio maana nasema Urusi... mmhh. Hasa kwa wale wanaopata scholarship za Kwenda huko.

5 comments:

Anonymous said...

Napita sana hapa ndugu yangu. Ila kimya kimya! Hongera kwa kazi ndugu yetu.

NDABULI said...

Aksante ndugu yangu,ila usipite kimya kimya kila wakati,kunijulia hali si vibaya kama leo :-)

Simon Kitururu said...

Ndabuli hapo Urusi wanaua weusi mpaka imekuwa kawaida. Lakini unaambiwa mpaka Marekani habari nyingi hupewa kazo akiwa Blondie mwenye macho ya blue. E bwana na mimi hupita sana hapa kimya kimya!Lakini nimeanza kuongea sasa:-)

Anonymous said...

while i agree that racism is an issue, students/visitors must be responsible for personal security; avoid some streets and dont stay out late.

View my homepage here

Anonymous said...

How can one be responsible for personal security, Anonymous, wakati hiyo njia unayopita kutoka shule - au usafiri unaotumia that particular day ndio majamaa yenye Xenophobia na racist wamejaa?

Lets now forget that we all have different pocket. There are those who have the pockets to afford a nice house in the surbabs and transportation that will assure them of security.

Lakini still, such doesn't promise anything. I lived in Botswana in the mid 80's - because of my father's line of work. Anyway, the first two houses we were to move - in the surbabs - to were planted with bombs.

Then I lived in South Africa, this time in the mid 90's - while I lived in a nice area with plenty security, my other (African)brothers who lived in the townships walikuwa kila siku wanasali maskini wakiwa wanatoka nyumbani.