Friday, October 13, 2006

UTAMKIKE KIRAHISI!...NA NANI?

Wiki hii ni wiki ambayo kutakuwa kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ni kumbukumbu ya kufikisha miaka saba tangu alipofariki dunia. Alifariki oktoba 14,1999. Langu mimi si kuzungumzia hizi kumbukumbu...sasa unataka kuzngumzia nini?
Nachotaka kuzungumzia ni kitu kingine kabisa ila kimeanzia kwenye Jina la Nyerere. Ni muda si mrefu ule uwanja wetu tunaoita wa kimataifa wa ndege Dar es salaam, ulibadilishwa jina na kuitwa Mwalimu Julius K. Nyerere International Airport. ...Sasa?..
Lakini sasa nimesikia kuwa eti wameondoa "mwalimu" na "K" ili utajike vizuri,.... ama!!! Utajike vizuri na nani sasa? Hapo kweli nimeshindwa kuelewa kuwa hawa watoa majina wanamtazamo gani? Kwani ni watanzania na wanaoongea kiswahili wangapi wanashindwa kutaja mwalimu! au K! Navyo fikiri mimi hata hilo jina lilivyobadilishwa lilikuwa halijatambuliwa sehemu nyingi ...kivipi?...
Umeisha wahi kujaribu kuangalia au kununua tiketi ya ndege katika mtandao,au kuangalia bei zake,au ratiba kwa safari zianziazo Dar es salaam au Kuishia hapo. Kwa kutumia huo utaratibu mashirika mengi ya ndege na makampuni wakala wa usafiri huwa wakionyesha sehemu uendapo na jina la kiwanja cha ndege lakini mpaka hvi karibuni sijaona ukitambuliwa kama mwalimu K. Nyerere....Sawa.. sasa wewe unachotaka kusema ni nini?
Lakini hili la kubadilisha ili litamkike nimeshindwa kulielewa kama ni kwa ajili ya nani? Kama ni kwa wageni wasiojua Kiswahili, kwanini wasijiufunze kutamaka hilo? sisi ndio tuwabadilishie kwa fadia ipi? Na wao mbona hata kubadilisha kutambua kuwa sio tena Dar es salaam international airport hawajafanya hivyo. Unajua airport moja Thailand inaitwaje? Suvarnabhumi International, Taiwani? unaitwa Taiwan Taoyuan International Airport , na mingine mingi tu inamajina kwa lugha yao. ..Kwa hivyo?... Ni wangapi unaowajua wewe wanaweza kutamka hayo majina? Umeishasikia watu hawataki kutumia uwanja kwasababu hawawezi kuutamka?.....MMMH.
Na kumbuka nimekutana na jamaa wengi wasio watanzania na katika kutambulishana nikisema mimi ni mtanzania utasikia oohh mwalimu nyerere!..... but what does mwalimu mean because I think it is not his really name? Basi inabidi kueeleza. Utasikia.... ooh thats interesting...
Mbona hawajabadilisha The mwalimu nyerere foundation iwe The Nyerere foundation. Hiyo foundation haitakiwi kutamkika? Tena nadhani hiyo ndio watu wantakiwa kuitaja sana maana NADHANI inatoa misaada.
Huu ndio mimi naona ni utumwa wa mawazo. Kwanini tusiendeleze kile tulichonacho? Ndio maana hata Raisi mstaafu wa msumbiji alituaibisha kwa yeye kuongea kiswahili wakati sio lugha rasmi katika nchi yake. Yeye akiwa mstari wa mbele kupigia chapuo lugha hii lakini wenyewe wenye kusema ndio lugha rasmi tuko kimya.Hili jambo linanifikirisha sana je ni utumwa wa akili au ni kutokujua?

2 comments:

Simon Kitururu said...

Mzee Ndabuli nakubaliana kabisa na wewe katika hili!Mimi nilishangaa sana kusikia kuwa etijina linabadilishwa ili liwe rahisi. Watu wamesaha hata jina langu kama Kitururu kwa Watanzania wasio na Rr ni gumu lina kuwa Kitululu. Wewe utakuwa Ndaburi nk. Sasa chakusikitisha zaidi ni kwamba jina limebadilishwa ili likidhi wageni basi mimi nikachoka kabisa hapo!

Anonymous said...

Ndabuli, nimependa uandishi wako. nimekunwa na maswali yako. Nadhani unan kichwa kizuri. Ulikuwa umekificha ehe?

Sijawahi kukusikia kabla hujaniandikia kwenye blogu yangu. Huoni kuwa huu ni wakati wa kutambulishana? Hebu jitambulishe vizuri ndugu yangu tujuane. Nimekufuata kwenye blogu yako, naona umejipa jina moja tu. Hivi kwa nini?