Wednesday, September 20, 2006

Daruso Hata Tovuti?

Katika kusoma soma kwa magazeti ya nyumbani katika mtandao ili angalau nijue kinachoendelea nimesoma kuna mgogoro Mkubwa sana kati ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam na Bodi ya mikopo. Jambo moja nililoliona ni ubishi wa gharama za maisha chuoni. Basi katika kutafakari mgogoro huu mawazo yangu yalinipeleka mbali sana. Nikajiuliza hivi Daruso ina tovuti yake? Hilo jambo sijaliona sasa najiuliza hivi hawa wasomi wetu wameshindwa kweli kutengeneza tovuti?Nikajisemea Hawa Daruso hawana tovuti, lakini wana miradi wanaendesha kwani hii miradi inawasaidia katika nini? Nimeona mifano ya vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu nchi nyingine vikiwa na uwezo wa kufungua migahawa yao ambayo inaendeshwa kwa bei za kiuanafunzi. kwanini wanafunzi wasijijenge kiuchumi ilikuondokana na Tatizo kama hili. Nielewavyo mimi hiki chama kipo kisheria na siku moja katika blogu ya bwana michuzi niliona picha moja ikionyesha jinsi eneo la chuo kikuu likiwa linaota majengo ya vitega uchumi, nikajiuliza hawa Daruso nao wananyanyua kitega uchumi chao ili kuondokana na huu mnyanaso nikasema sidhani kama tovuti hawana itakuwa ili wazo. Je, kweli tutaweza kujisadia wenyewe?

5 comments:

mloyi said...

Karibu kwenye ulimwengu huu wa blogu, sisi tupo na ndiyo tunavyoishi, Dunia hii ya kuhangaika na kuzunguka huku na kule tunaiishi, hivi ndiyo huwa tunakutana na kuongea masuala yetu.
Ndiyo tulivyo, Tunaangalia sana pale kwenye pesa tuu!
Sijui DARUSO inaelekea wapi? au shughuli zake ni kuongoza migomo tuu, kwanini hawakui? inashangaza sana.
Cha kusikitisha, kuna wanafunzi wanasomea Ukokotozi wa kisayansi, na hiyo ni moja ya kazi zao lakini hawana nusu saa kwa wiki kushughulikia tovuti ya daruso, hawaangalii kama hiyo itaonyesha ukomavu wao kielimu wanayoipata hapo na vilevile ni moja ya mafunzo kwa vitendo na inakuza CV zao.
Chamgamoto kubwa kwa wahusika nadhani watapitia kwenye blogu yako.

Egidio Ndabagoye said...

Karibu8 sana kaka utupatie mavitu mapya mapya.Kaka Mloyi kasema kuwa "Cha kusikitisha, kuna wanafunzi wanasomea Ukokotozi wa kisayansi, na hiyo ni moja ya kazi zao lakini hawana nusu saa kwa wiki kushughulikia tovuti ya daruso, hawaangalii kama hiyo itaonyesha ukomavu wao kielimu wanayoipata hapo na vilevile ni moja ya mafunzo kwa vitendo na inakuza CV zao".
Sasa cha kuchekesha na kusikitisha zaidi hao wanaojifunza taaluma hiyo ya ukokotozi hata ukiwauliza ile introduction ya kompyuta hawajui.Jamaa mmoja alinianbia kuwa pale katika taaluma hiyo utumniaji wa kompyuta kwa vitwendo nikama vile hakuna.Inabidi waende kupata mafunzo ya vitendo katika vyuo vya mitaani.Hilo ndilo jibu lao.

Wenzao wa mzumbe wako mtandaoni huu http://www.mumuso.itgo.com/

NDABULI said...

Bwana Mloyi na Egidio Nashukuru kwa Karibu yenu.Nakumbuka ule msemo (sijui unapatikana wapi)kwamba Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
Egidio nifikishie hongera zangu kwa hao wa Mzumbe

mwandani said...

Ndugu zangu tukaze nia. Naomba gurudumu hili la fikra endelevu liambatane na vitendo.

katika kila gazeti tando haupiti muda bila kuhimizana kufuatilia masuala ya maendeleo kwa vitendo.

Wakati ni huu, hatua baada ya hatua.

Karibu ukumbini.

NDABULI said...

Nimekaribia Mwandani