Monday, April 23, 2007

Nimerudi tena Jamani. Baada ya kufuta vumbi nyumbani na kusalimia mtaani nikaona ngoja niwabeep (au niwa dipu kama anavyosema Chesi Mpilipili) wale walionitembelea wakati sipo na kuacha ujumbe na wale waliopita kimyakimya. Katika mihangaiko yangu nilifika pale Parisi, Ufaransa na nilitembelea ule mnara wao maharufu (ingawa walitaka kuuondoa mwanzoni) wa Eiffel. Kilichonifurahisha pale Kileleni niliona wameonyesha ni umbali gani uliopo kutoka Hapo Kileleni hadi Mwanza na Dar es salaam.
Angalia pale juu kileleni ndio kuna hayo maandishi hapa chini



Huu ni umbali Kutoka Kileleni mwa mnara wa Eiffel Kuelekea Mwanza.



Na huu ni umbali Kuelekea Dar es salaam.





8 comments:

Egidio Ndabagoye said...

Karibu tena mkuu.Ulienda kupiga kura nini?(Natania).Tupatie nyepesi nyepesi za Parii

Simon Kitururu said...

Karibu tena Mzee!Halafu huo mji unasifa zake nyingi nzuri lakini walalahoi wake na sehemu wanazoishi huzisikii.Ni paka wakileta madai Mtaani ndio wengi wanastukia, ala kumbe walalahoi na mitaa yao ipo.

NDABULI said...

Egidio: bado kidogo nilazimishwe kupiga Kura! maana upinzani ulikuwa mkali:), ilitokea tu harakati zangu ziligongana na mambo ya uchaguzi.
Simon: Nakwambia huo mji kuna sehemu ukienda hakuna tofauti na baadhi ya sehemu za nyumbani tena na nyumbani inakuwa afadhali.

MTANZANIA. said...

Ndabuli!
Nilikuwa sijastukia ka umerudi. Tunasubiri vituzi.

Christian Bwaya said...

Ndabuli,
unafanya kazi nzuri sana. Blogu yako inavutia na vikolezo vyake vinaweza kumfanya mtu asahau kazi nyingine akabaki humu humu ndani.

Njia hii ya kuacha ujumbe kama wa yule mama wa Vodacom...inafaa!

mzee wa mshitu said...

Karibu kaka nasiki umeshiriki kuiba kura huko Paris hadi hii kambi na nanihii ikawa inawapiga bao wenzao, anyway utani enhee mambo vipi mzee, sijaelewa huu mnara unasema una kakibao juu yake ambako kameandikwa Tanzania au?? Nasikia Paris kuna sehemu wanapika ugali kama bongo tena mtamu kichizi

NDABULI said...

BWAYA na wewe Karibu tena, ni siku nyingi nilikuwa napita kwako lakini nakuta kimya,ila naona umeamua kurudi..Karibu Tena.
MTANZANIA nimerudi ndio najaribu kutuliatulia..
CHARAHANI. yaani hiyo parii ni kweli kuna sehemu unapata msosi kama ule wa pale polisi ukitoka utawala(chuo),na imegawanyika kupo kwa walalahoi na kwa wenyezao tofauti ni kubwa unapotoka sehemu moja kwenda nyingine,nilijaribu kutembelea sehemu moja ya wahamiaji ilibidi safari iishie mwanzoni maana mwenyeji wangu aliiona huko unawezapigwa roba ya mbao (yeye na uwenyeji wake alikuwa hajawi fika huko..na walikuwa wakimshangaa)
Kuhusu kibao Kule juu kabisa ya mnara kuna chumba kinachozunguka mnara huko ndani ndio kuna hivyo vibao.

Simon Kitururu said...

Duh!Mzee umetupotea tena!