Friday, March 30, 2007

IMANI ZETU INAKUWAJE?

Siku moja (Miaka kadhaa iliyopita baada ya septemba 11 ya marekani) nikiwa katika daladala, si unajua kwenye dala dala (hasa vipanya,ila niliyokuwa mimi ilikuwa ngarangara) mtu anaweza akaanzisha hoja/swala/hadithi/mchapo/swali ambalo abiria wote ndani ya daladala wanaanza kuchangia kila mtu kwa mtazamo wake... basi nikiwa ndani ya hilo dala dala ilikuwa usiku umeingia na jamaa wengi ndani ya dala dala walikuwa wanaonekana kuchoka kutokana na mihangaiko ya siku basi walikuwa kimya ila kulikwa na bwana mmoja alikuwa nadhani Kasimu wa matumizi (....unaporudi nyumbani unamwambia mama watoto pesa zote umeibiwa....NADHANI UNANIELEWA HAPA KWA WASIOELEWA ALIKUWA AMELEWA POMBE) basi jamaa yule kweli zilikuwa zimemkamata (ila sikuwa na uhakika ni za aina gani alikuwa amekunywa maana mimi nilikuwa mbali nae kidogo hivyo ile harufu haikunifikia ) kama kawaida ya makonda nao huwa hawachelewi kwa kejeli zao, basi konda aliendelea na kejeli kwa bwana Kasimu wa matumizi, yule jamaa baada ya kuona ni yeye tu na konda wanaobishana na yeye kuelekea kushindwa aliamua kutugeukia abiria,.... basi akaanza hivi...!
Kasimu wa matumizi:Unajua watu wengi wanamuona mmarekani hawapendi waiisalamu, lakini nyie hamjui ....
Konda: Kwanini?Mmarekani bwana hawapendi waisalamu si unaona anavyowafanyia?
Kasimu wa matumizi: aaa mmarekani bwana hana cha muislamu wala mkristo..... nyie si mnasema anawaonea waislamu angalia sasa alivyowafanyia wakristo amewachagulia wakristo askofu SHOGA halafu kawaambia mtake msitake huyu ndiyo askofu, wakristo wote jasho linawatoka...
Nakwambia basi lote tulitokwa na kicheko na mjadala ukaanza.
Basi lengo la hadithi hii ni kuangalia mstakabali huu wa dini zilizoletwa na hawa wageni kwetu, sasa hivi tunaona jinsi dini zilivyo katika migogoro.Ya ukristo.., Kanisa la Kianglikana lina mtafaruku mkubwa hasa umegawanyika kati ya viongozi wa kanisa kutoka Afrika na wale wa Marekani kuhusu swala la ushoga, makanisa yanatishia kukataa misaada toka kwa makanisa ya Kishoga, juzi juzi kanisa la Uswidi nalo limesema litakuwa linabarikia ndoa za mashoga soma hapa (hili ni kanisa la kilutheri )sasa sijui waluteri watanzania wanasemaje?
Ya uislamu kuna wale washia na wale wa sunni ni vurugu tupu..
Kuna rafiki yangu mmoja nae siku moja wakati tukipata moja moto ,moja baridi na moja ya uvuguvugu (kwenye mgahawa wa chuoni tulipokuwa tunasoma) akawa na ubishi na jamaa mmoja alikuja kutuhubiria kuwa hizi mojamoto, moja baridi, na moja ya uvuguvugu hazifai kwa jina la yesu. Basi jamaa akasema mbona kwenye hiyo biblia uliyoshika kuna sehemu imeandikwa kuwa Yesu alitengeneza kinywaji kwenye harusi maana watu mtindi ulikuwa umewaiishia na harusi ikaanza kuwa hakieleweki kitu.. basi jamaa akaanza kutoa maelekezo kuwa oo ile ilikuwa haina kilevi... Kumkatisha jamaa iliaaondoke... (nasi tunendelee na moja yenye umande)basi yule bingwa wangu akamwambia jamaa afadhali waisilamu bwana wao Koran yao imeandikwa Kiarabu na haibadilishwi nyie biblia yenu iko katika kila lugha basi inakuwa mtafaruku maana kila mtu na tafsiri yake...
Kumbuka lakini hawa jamaa wanatoa maoni yao wakati akili yao inaushawishi wa pombe.
Lengo langu mimi nikujiuliza hivi kwanini hawa jamaa walivyokuja kututawala wakasema imani zetu potofu, watu wakakubali bila kujiuliza. Mbona wao hawajafuta imani zao za zamani mpaka leo. Si unajua yale majina ya sayari kwa Kimombo ni majina ya miungu ya Kigiriki? si unajua neno victory linatokana na Mungu wa Kirumi soma hapa . Sina unajua Nike naye alikuwa mungu wa Kigiriki soma hapa.
Basi Lengo langu mimi nikuzungumzia imani zetu za kijadi ambazo nitaendelea nazo Makala ijayo..

5 comments:

Evarist Chahali said...

Mzee,nimepita hapa na kwa hakika nimepata stori mwanana sana.
Bonge

mzee wa mshitu said...

kaka umenikumbusha maisha ya hapa bongo kumbe hujasahau, hali unayoizungumzia ndo hasa ipo ya kina kassimu wa matumizi na makonda wao, lakini kikubwa hii mada unayoizungumzia ni relevant kabisa kaka, baab k mambo vipi lakini huko kwenu.

MTANZANIA. said...

Ni vema baadhi ya mambo yetu ya asili yakaendelezwa katika mfumo wa usasa zaidi. Ninachokisema hapa ni kwamba "ule uasilia ubaki palepale hata kama kuna vikolombwezo"
Hadirhi tamu mkuu!

Simon Kitururu said...

Hadithi tamu Mzee lakini ujumbe kiboko. Ila mimi nachokataa ni jinsi watu wanavyorahisisha mambo. Ni rahisi kusikia watu wakisema kuwa migogoro ya wakristo inatokana na tafsiri za biblia kuwa katika lugha nyingi. lakini ukiamini hivyo unasahau kuwa migogoro mingi ya kiislamu pia iko katika tafsiri ya Kitabu ingawa hata wagombanaji wanatumia kitabu chenye lugha moja. Lakini kuna nchi zimeanza kufundisha Uislamu kwa lugha nyingine.Spain ni mojawapo. Dini nyingi duniani pamoja na kuhubiri amani , zinaanzisha vurugu kutokana na watu wazielewvyo. Chakusikitisha ni kuwa dini nyingi kufunza wafuasi kuwa zenyewe ndio za kweli za wengine ni za uongo. Halafu moja ya mapungufu ya dini ni kwamba , asilimia kubwa ya watu huamini katika dini waliozaliwa wakajikuta ndani yake.Na hiyo huwaambia kuwa wengine wamepotea. Wachache hujitoa na kufikiria maswala ya dininyingine bila kuweka msingi wakutathmini dini nyingine katika misingi ya dini aijuayo. Basi hapo ndio kasheshe. Imani ni kitu fulani nakiogopa sana.Jina rahisi mambo yake makubwa

NDABULI said...

@BONGE nafurahi kwa kunitembelea hapa barazani.
@CHARAHANI(mt-----u!)kusahau maisha unayopitia si rahisi,naona kalamu yako inafanya kazi kwelikweli,nitapita kutoa tongotongo siku za karibuni.
@MTANZANIA nakubaliana na wewe ila ule usasa usiwe umagharibi au Ulaya au Uarabu
@KITURURU na wewe umesema kweli haya magomvi naona yanatokea kwa sababu hivi vitu sisi sio asili yetu,sijasikia au kusoma historia(ingawa nayo nyingi iliandikwa na haohao)kuwa zile imani zetu zilikuwa na kutokuelewana namna hii inavyoonekana sasa.