Monday, July 30, 2007

CHAI,ZAMBARAU NA FULLLIGHT !

Anti: Karibuni, Karibuni,Karibuni ngoja niwaongezee kiti
Ndabuli: Asante Anti, du anti umependeza!
Washikaji wa Ndabuli: Wanacheka..
Anti: We anko(anamjua jina lake) unacheka nini sasa?
Mshikaji 1 wa Ndabuli: Yaani we Hadija leo unaniita anko?
Mshikaji 2 wa Ndabuli: Hube tulete vinywaji hizo longolongo zenu mtaongea wakati tunakata kiu.
Anti: Anko unakuywa nini?
Ndabuli: Naombaaa (nasitasita)....
Mshikaji 2: Kunywa Kilimanjaro au Tusker
Mshikaji 1: Kunywa Serengeti ndio yenyewe...mletee Serengeti darling wangu!
Anti: (Huku anacheka) Koma wee mie Darl wako leo, (anagongea mkono pwaa na mshikaji 2 )sitaki kabisa utani wako, haya sema na wewe unakunywa nini?

Mshikaji 1: (tena kwa msisitizo na sauti kubwa)Kahawa !
Anti: Kha, unanini leo wewe, mkeo leo kakufumania nini au umerukwa na akili wewe.
Ndabuli: Kwani hamuuzi kahawa hapa?
Woote jirani yetu: Wanacheka !haha haha! haha!

Basi nisiendelee sana ngoja niseme...mmhh hapana niandike, hadithi inataka niseme nini? Huku ugenini kwenye sehemu ya kinywaji unaweza pata Kahawa, chai. Sasa katika safari yangu ya nyumbani katika maongezi na ndugu jamaa na marafiki tulifika wakati tukaongelea hili jambo basi tukasema hebu tukiwa siku moja tunakwenda kupooza koo tujaribishe halafu tuone itakuwaje..basi ndio ikawa hiyo watu walibanwa mbavu kwa kucheka-
Basi mjadala ukaanza.... kwanini wasiuze kahawa na chai hapa-nakwambia kila upande ulielekea kushinda...
Ila swala langu ni moja tuliweza kuanzisha mjadala ambao wengi wetu tulichangia na kuendelea kupooza koo kwa furaha kabisa (na mpaka mwenye sebule ile tukamwambia ajaribu kuaanza hii biashara tuone itakuwaje?)..Ntaendelea na hiki Kisa baadae

Umeisha safiri na kwa kutumia Barabara kutoka mkoa mmoja hadi mwingine? Si unakumbuka kuona madereva wanawashiana taa au kupungiana mikono huku wakionyesha alama fulani? ..na wanaelewana hebu jiulize au waulize kama walifundishwa maana zake wakati wa mafunzo ya udereva... aaa wapi? Lakini mbona wanaelewana... na hili nitalimalizia baadae

EGIDIO Kaniuliza mambo 8 msiyoyajua juu yangu.

1. Sijui vitu vyote msivyojua kuhusu mimi.
2. Naogopa sana mkijua vitu msivyojua kuhusu mimi.
3. Naogopa sana kupigwa picha.
4. Akina Dada wote naokuwa na urafiki(wa kimw....) na mimi (akina Stella)baada ya muda(au tukimalizana) wanaolewa. ...mhh mwajameni!
5. Akina stella wangu wote tuliokuwa pamoja tulianza ghafla urafiki.
6. Napenda sana Kula chips dume(mihogo ya Kukaanga).
7. Nilisimamishwa shule kwa mara ya Kwanza nikiwa darasa la nne.(Kwa sababu ya kugoma kuchapwa viboko nikiwa nimevua kaptura mbele ya wasichana- nilikamatwa nimepanda mti nikidondosha zambarau!) ...mmh mwanawane!
8. Rejea namba mbili.

Alamsiki